• HABARI MPYA

    Sunday, December 14, 2025

    TAIFA STARS YAICHAPA HARAS EL HODOOD 1-0 MECHI YA KIRAFIKI MISRI


    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' jana iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya klabu ya Haras El Hodood SC katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Jeshi la Anga June 30 Jijini Cairo nchini Misri.
    Katia mchezo huo wa kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21 hadi Januari 18, mwakani bao pekee la Taifa Stars lilifungwa na kiungo wa Simba SC, Morice Michael Abraham.
    Taifa Stars imeweka kambi nchini Misri kujiandaa na AFCON hadi Desemba 18 itakapoondoka kwenda Morocco tayari kwa Fainali hizo hizo za 35 za Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Taifa Stars ambayo inashiriki Fainali hizo kwa mara ya nne baada ya 1980 Nigeria, 2019 Misri na 2023 Ivory Coast — imepangwa Kundi C pamoja na Nigeria, Tunisia na Uganda.
    Katika Fainali zote zilizotangulia Taifa Stars imekuwa ikitolewa hatua ya makundi - tena bila kushinda mechi hata moja wakitoa sare na kufungwa.
    Mwaka 1980 walifungwa 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri pamoja na Sara ya 1-1 na Ivory Coast, 2019 walifungwa mechi zote, 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria — wakati mwaka 2023 walifungwa mechi moja, 3-0 na Morocco na sare za 1-1 na Zambia na 0-0 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAICHAPA HARAS EL HODOOD 1-0 MECHI YA KIRAFIKI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top