• HABARI MPYA

  Thursday, September 20, 2018

  MAMBO YA WACHEZAJI WA YANGA AMBAYO YANAMKERA KOCHA MWINYI ZAHERA ILE MBAYA

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  LICHA ya kikosi cha Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union na kuchukua pointi tatu kisha kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameonekana kutoridhishwa na kiwango cha wachezaji wake.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Zahera amesema wachezaji wake wamekuwa na makosa mengi sana ya wazi yanayosababisha timu hiyo kutoka na ushindi mwembamba uwanjani.
  “Wachezaji hawabadiliki angalia mchezo dhidi ya Algeria (USM Alger), mechi dhidi ya Mtibwa (Sugar), dhidi ya Stand (United) na hii,  tumekuwa na ushindi wa mabao 2-0, 2-1, 4-3,”.
  “Tatizo la wachezaji wangu hawana umakini tunapata goli tunakuwa kama watoto, wachezaji wanafanya vitu vya hovyo mwangalie  Makambo  (Heritier), mshambuliaji unapewa mpira unarudisha nyuma,” alisema Zahera.

  Kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera (katikati) haridhishwi na kiwango cha wachezaji wake

  Hata hivyo, Zahera amemsifu kiungo Ibrahim Ajib kwamba kwa sasa amekuwa ana msaada kwenye timu tofauti na awali. Amesema Ajib amekuwa na utulivu uwanjani hali inayomsababisha kucheza 
  vizuri.
  “Ajibu amebadilika si yule wa kucheza na kushindwa kufunga anapata mpira na kufunga na amekuwa na nidhamu ya mpira,” alisema Zahera.
  Yanga inaongoza ligi kwa pointi tisa baada ya ushindi wa jana dhidi ya Coastal Union, Azam FC wametoka suluhu jana dhidi ya Biashara United ikiwa ni sare ya pili. Mchezo wa Simba na Mbao FC unachezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ndiyo utakaoamua timu gani ibaki kileleni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMBO YA WACHEZAJI WA YANGA AMBAYO YANAMKERA KOCHA MWINYI ZAHERA ILE MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top