• HABARI MPYA

    Thursday, September 20, 2018

    AFRICAN LYON YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAICHAPA SINGIDA UNITED 3-2, PRISONS SARE TENA SOKOINE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya African Lyon imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwalaza 3-2 Singida United katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
    Ushindi huo unaifanya timu ya Rahim Kangenzi ‘King Zamunda’ kufikisha pointi sita baada ya kucheza mechi tano, nne za awali ikitoa sare tatu na kufungwa moja, wakati SU inabaki na pointi zake saba baada ya kucheza mechi tano.
    Katika mchezo wa huo, mabao ya African Lyon yamefungwa na Said Mtikila dakika ya 50, Mbrazil Victor Da Costa dakika ya 70 na Ismail Gambo dakika ya 75, wakati ya Singida United yamefungwa na Hans Kwofie dakika ya 57 na Habib Kiyombo dakika ya 62.  
    Mshambuliaji Mbrazil wa African Lyon, Victor Da Costa akipambana na beki wa Singida United leo

    Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbao FC wameifunga Simba SC 1-0, bao pekee la Said Khamis Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wakati Tanzania Prisons imelazimishwa sare ya 2-2 na Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
    Prisons walitangulia kwa mabao ya Salum Kimenya dakika ya 37 na Hassan Kapalata dakika ya 53, kabla ya Kagera Sugar kuzinduka na kusawazisha kupitia kwa Paul Ngalyoma dakika ya 82 na Ramadhani Kapera dakika ya 85.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFRICAN LYON YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, YAICHAPA SINGIDA UNITED 3-2, PRISONS SARE TENA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top