• HABARI MPYA

    Wednesday, April 08, 2026

    SINGIDA BLACK STARS YAZINDUKA NA KUICHAPA KMC 1-0 AIRTEL MWIGULU


    TIMU ya Singida Black Stars imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Airtel Mwigulu mjini Singida.
    Bao pekee la
    Singida Black Stars katika mchezo wa leo limefungwa na winga Mgambia, Lamine Jarjou dakika ya 70 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 28 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya tano.
    Kwa upande wao KMC hali inazidi kuwa mbaya baada ya kupoteza mchezo wa leo wakiendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16 kwa pointi zao nane za mechi 18.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAZINDUKA NA KUICHAPA KMC 1-0 AIRTEL MWIGULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top