TIMU za Azam FC na Simba SC zimetoshana nguvu kwa sare ya bila mabao katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Ulikuwa mchezo mzuri wa kiufundi na maarifa, timu zote — Azam FC inayofundishwa na Kocha Mkongo Jean-Florent Ikwange Ibenge na Simba SC ya Kocha raia wa Afrika Kusini, Steven Robert Barker zikishambuliana kwa zamu.
Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 33 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidwa pointi mbili na Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Ikumbukwe, mabingwa watetezi, Yanga SC ndio wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 41 za mechi 17.



.png)
0 comments:
Post a Comment