• HABARI MPYA

    Sunday, April 05, 2026

    TRA UNITED YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-0 ARUSHA


    TIMU ya TRA United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Mabao ya TRA United yote yamefungwa na mabeki, mzawa Abdallah Kheri ‘Ssebo’ aliyejifunga dakika ya 10 na Mganda Christopher Tebandeke kwa penalti dakika ya 40. 
    Kwa ushindi huo, TRA United inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 17 ikisogea nafasi ya nane kutoka ya 10, wakati Singida Black Stars inabaki na pointi zake 25 za mechi 17 sasa ikisalia nafasi ya sita.
    Baada ya mchezo huo, Singida Black Stars imetangaza kuondoa Maafisa wote wa benchi lake la Ufundi kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TRA UNITED YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-0 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top