• HABARI MPYA

    Sunday, December 14, 2025

    WOLVES WAIFUNGIA ARSENAL MABAO MAWILI IKIWACHAPA 2-1 LONDON


    WACHEZAJI wa Wolverhampton Wanderers jana walijifunga mara mbili kuisaidia Arsenal kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
    Alianza kipa Muingereza Samuel Luke Johnstone kujifunga dakika ya 70, kabla ya beki Mcolombia, Yerson Mosquera Valdelamar kujifunga naye dakika ya 90'‎+‎4.
    Bao pekee la Wolverhampton Wanderers likifungwa na mshambuliaji Mnigeria Toluwalase 'Tolu' Emmanuel  Arokodare dakika ya 90.
    Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 36 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi nne zaidi ya Manchester City, wakati Wolverhampton Wanderers inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 20 ikibaki na pointi zake mbili baada ya timu zote kucheza mechi 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WOLVES WAIFUNGIA ARSENAL MABAO MAWILI IKIWACHAPA 2-1 LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top