MSHAMBULIAJI Mfaransa mwenye asili ya Cameroon, Hugo Timothée Ekitike jana alifunga mabao yote mawili dakika ya kwanza na 60 Liverpool ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield, Liverpool.
Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 26 na kusogea nafasi ya sita ikiizidi pointi tatu sasa Brighton & Hove Albion FC baada ya timu zote kucheza mechi 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment