TIMU ya Argentina imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Cape Verde katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Hard Rock Jijini Miami Gardens, Florida nchini Marekani.
Mabao ya Argentina yamefugwa na mshambuliaji wa Inter Miami ya Marekani, Lionel Andrés "Leo" Messi dakika ya 29 na mabeki wa kati, Lisandro Martínez wa Manchester United ya England dakika ya 92 na Edilson Alberto Monteiro Sanches Borges wa Al Bataeh ya Falme za Kiarabu (UAE) aliyejifunga dakika ya 111.
Kwa upande wao Cape Verde mabao yao yamefungwa na wachezaji wake waliozaliwa Uholanzi, kiungo wa Ludogorets Razgrad ya Bulgaria, Deroy d'Encarnação Duarte mzaliwa wa Uholanzi dakika ya 59 na beki wa pembeni wa Trabzonspor ya Uturuki, Sidny Lopes Cabral dakika ya 103.



.png)
0 comments:
Post a Comment