• HABARI MPYA

  Thursday, September 20, 2018

  RUVU SHOOTING WADAI NYEKUNDU NDIYO ILIYOWAPONZA KUPIGWA NNE NA MBEYA CITY JANA

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Ruvu Shooting jana kilishuka kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City na kufungwa mabao 4-2.
  Katika mchezo huo, wachezaji nane wa Ruvu Shooting walizuiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kucheza kutoka na vibali vyao kuchelewa kutoka.
  Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kikosi cha timu yake kilikua na wachezaji 12 ambapo 11 walianza na mmoja ambaye ni beki alibaki akiwa ni mchezaji wa akiba.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – online, Bwire amesema licha ya kikosi hicho kuwa na wachezaji wachache, dakika za mwanzoni kabisa za mchezo huo mchezaji wao Ayoub Kitala alitolewa na mwamuzi kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga Nchunga Said wa Mbeya City.
  Ruvu Shooting jana imechapwa mabao 4-2 na Mbeya City Uwanja wa Sokoine

  Alisema kadi hiyo nyekundu iliwatoa mchezoni wachezaji wote kutoka mchezoni na kuruhusu mabao yote manne. “Tumesafiri Mbeya na wachezaji 18 lakini kati yao wachezaji nane TFF ikasema hawana sifa ya kucheza, nimehangaika kuja Shirikisho lakini kati ya hao wachezaji wawili ndiyo waliopata kibali cha kucheza.
  “Hivyo tukawa na jumla ya wachezaji 12 watakaocheza dhidi ya Mbeya City na mmoja wao akapewa kadi nyekundu mwanzoni mwa mchezo hali iliyowatoa mchezoni wachezaji na viongozi,” alisema Bwire.
  Licha ya wachezaji nane kuzuiliwa na TFF kuitumikia Ruvu Shooting,  timu hiyo ina jumla ya wachezaji nane wengine ambao ni majeruhi ambao wameshindwa kuitumikia timu yao katika mechi dhidi ya Mbeya City.
  Licha ya kichapo hicho, Bwire ameitangazia kilio Coastal Union ambayo watakutana nayo katika mchezo wao ujao utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini Jumamosi wiki hii Septemba 22.
  “Mchezo unaokuja tutakuwa Mabatini dhidi ya Coastal Union nina imani wale wachezaji nane walio majeruhi watakua wamerejea katika afya njema, tuko vizuri tuko sawasawa na tutafanya makubwa nina uhakika umahiri wetu wa papasa squared utaanza kuonekana hapo na kufuta yote yaliyotokea katika michezo iliyotangulia,” alisema Bwire.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING WADAI NYEKUNDU NDIYO ILIYOWAPONZA KUPIGWA NNE NA MBEYA CITY JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top