TIMU ya Yanga ya Tanzania imepangwa Kundi pamoja na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Al Hilal ya Sudan na MC Alger ya Algeria katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kundi B linaundwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Raja Club Athletic, maarufu kama Raja Casablanca, AS FAR Rabat, zote za ya Morocco na AS Maniema Union ya DRC.
Kundi C linaundwa na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Stade d'Abidjan ya Ivory Coast, wakati Kundi D kuna Espérance ya Tunisia, Pyramids ya Misri, Djoliba ya Mali na Sagrada Esperança ya Angola.
0 comments:
Post a Comment