BAO pekee la beki Heritier Lulihoshi dakika ya 71 kwa penalti jana liliipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inayofundishwa na kocha Mecky Mexime inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya saba, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi tisa.
0 comments:
Post a Comment