• HABARI MPYA

    Wednesday, April 16, 2025

    YANGA NA KVZ, AZAM NA KMKM ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI


    VIGOGO, Yanga watamenyana na wenyeji, KVZ katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Muungano Aprili 25 kuanzia Saa 2:15 usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Robo Fainali nyingine ya michuano hiyo itazikutanisha wenyeji, JKU na Singida Back Stars Aprili 23, wenyeji, Zimamoto na Coastal Union Saa 10:15 na wenyeji wengine, KMKM dhidi ya Azam FC kuanzia Saa 2:15 usiku Aprili 24 Uwanja wa New Amaan Complex pia.
    Nusu Fainali zitafuatia Aprili 27 na 28, wakati Fainali itachezwa Aprili 30 hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex.


    Mabingwa watetezi, Simba wameshindwa kushiriki michuano ya mwaka huu kwa sababu wanakabiliwa na mechi za Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini Aprili 20 nyumbani na Aprili 27 marudiano ugenini.
    Simba SC ilitwaa michuano hiyo iliyoanza mwaka jana kuzimisha sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika Fainali Uwanja wa New Amaan Complex.
    Bao pekee la Simba lilifungwa na kiungo Msenegal, Babacar Sarr, dakika ya 77 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Israel Patrick Mwenda kufuatia mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana kuangushwa nje kidogo ya boksi.
    Simba SC ilizawadiwa Sh. Milioni 50, wakati washindi wa pili, Azam FC walipata Sh. Milioni 30. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA KVZ, AZAM NA KMKM ROBO FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top