• HABARI MPYA

    Saturday, April 19, 2025

    SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 LITI


    WENYEJI, Singida Black Stars wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM LITI mjini Singida.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Niger, Victorien Adebayor Zakari Adje dakika ya 21 na mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah, mawili dakika ya 52 kwa penalti na 86.
    Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 27 na kusogea nafasi ya pili, ikiizidi pointi mbili Azam FC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi na muda huu wapo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wanacheza na wenyeji, Kagera Sugar.
    Kwa upande wao Tabora United pamoja na kupoteza mchezo wa leo wanabaki nafasi ya tano na pointi zao 37 wakiizidi pointi tatu Dodoma Jiji FC baada ya timu zote kucheza mechi 27.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top