WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Abdallah Said dakika ya sita na Rashid Chambo dakika ya 28 — na la Dodoma Jiji limefungwa na Iddi Kipagwile dakika ya 39.
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 26 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 34 za mechi 27 nafasi y sita.
0 comments:
Post a Comment