• HABARI MPYA

    Wednesday, April 23, 2025

    SERIKALI YAGHARAMIA USAFIRI NA MALAZI SIMBA SC MARUDIANO NA STELLENBOSCH


    SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Dk. Samia Samia Suluhu Hasan imegharamia usafiri na malazi kwa klabu ya Afrika kwenye mchezo wake wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Stellenbosch Jumapili.
    Katika barua yake ya shukrani kwa Rais Samia, Rais wa Simba SC, Mohamed 'Mo' Dewji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi amesema; "Tumepokea kwa moyo wa shukrani mchango wa malazi na usafiri kuelekea mchezo wetu wa marudiano wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaofanyika Afrika Kusini,".


    Mo Dewji ambaye ni Mbunge wa zamani wa jimbo la Singida mjini ametoa shukrani pia kwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi nzuri ya kuratibu safari hiyo. 
    Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo kwa ndege maalum ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) waliyopewa na Serikali kikiwa na  wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni pia Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban.
    Simba SC inahitaji sare ya aina yoyote kukata tiketi ya Fainali baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Jumapili ya juzi Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45'+2 kwa shuti la kitaalam la mpira wa adhabu lililomshinda kipa wa Afrika Kusini, Oscarine Masuluke.
    Mshindi wa jumla Kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria katika Fainali.
    Ikumbukwe RSB Berkane ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90'+2 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAGHARAMIA USAFIRI NA MALAZI SIMBA SC MARUDIANO NA STELLENBOSCH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top