MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefuzu Raundi ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Copco United ya Mwanza leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na kiungo mzawa, Shekhan Ibrahim Khamis dakika ya 35, mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 57, viungo Mkongo Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 68 kwa Penalti, Mkenya Duke Ooga Abuya dakika ya 77 na Mudathir Yahya Abbas dakika ya 84.
Yanga inaungana na timu za Mbeya City, Green Warriors, TMA Stars, Namungo FC, JKT Tanzania, Cosmopolitan, Polisi Tanzania, Town Stars, Stand United, KMC, Pamba Jiji, Fountain Gate, Coastal Union, Leo Tena, Azam FC, Transit Camp, Biashara United, Mtibwa Sugar, Songea United, Mashujaa FC, Singida Black Stars, Mambali FC, Kagera Sugar, Geita Gold, Giraffe Academy, Mbeya Kwanza, Kiluvya FC, Tanzania Prisons, Big Man FC na Tabora United zilizotinga 32 Bora.
Timu ya 32 itapatikana kesho baada ya mchezo wa mwisho wa Raundi ya Tatu kati ya Simba na Kilimanjaro Wonders SC hapo hapo Uwanja wa KMC Complex.
0 comments:
Post a Comment