TANZANIA imepangwa Kundi C katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zitakazofanyika kuanzia Desemba 21 mwaka huu hadi Januari 18 mwakani, 2026 pamoja na jirani zao, Uganda, Tunisia na Nigeria.
Katika Droo ya upangaji makundi ya AFCON 2025 iliyofanyika usiku wa Jumatatu ukumbi wa Mohammed V National Theatre Jijini Raba nchini Morocco, wenyeji wa Fainali hizo wapo Kundi A pamoja na Mali, Zambia na Comoro, wakati mabingwa watetezi, Ivory Coast wapo Kindi F pamoja na Cameroon, Gabon na Msumbiji.
Kundi B linazikutanisha Misri, Afrika Kusini, Angola na Zimbabwe, wakati D kuja Senegal, DRC, Benin na Botswana na Kundi E wapo Algeria, Burkina Faso, Equatorial Guinea na Sudan.
MAKUNDI YOTE AFCON 2025 MOROCCO
KUNDI A: Morocco, Mali, Zambia, Comoro
KUNDI B: Misri, Afrika Kusini , Angola, Zimbabwe
KUNDI C: Nigeria, Tunisia, Uganda, Tanzania
KUNDI D: Senegal, DRC, Benin, Botswana
KUNDI E: Algeria, Burkina Faso, Equatorial Guinea, Sudan
KUNDI F: Ivory Coast, Cameroon, Gabon, Msumbiji
0 comments:
Post a Comment