TIMU ya Simba SC imekamilisha idadi ya timu 32 za Raundi ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Kilimanjaro Wonders leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na Valentino Mashaka dakika ya kwanza, Ladack Chasambi dakika ya nne, Patrick Sebastian aliyejifunga dakika ya tisa, Mzambia Joshua Mutale dakika ya 21, Mganda Steven Mukwala dakika ya 48 na Edwin Balua dakika ya 80.
Simba inaungana na mabingwa watetezi, Yanga, Mbeya City, Green Warriors, TMA Stars, Namungo FC, JKT Tanzania, Cosmopolitan, Polisi Tanzania, Town Stars, Stand United, KMC, Pamba Jiji, Fountain Gate, Coastal Union, Leo Tena, Azam FC, Transit Camp, Biashara United, Mtibwa Sugar, Songea United, Mashujaa FC, Singida Black Stars, Mambali FC, Kagera Sugar, Geita Gold, Giraffe Academy, Mbeya Kwanza, Kiluvya FC, Tanzania Prisons, Big Man FC na Tabora United zilizotinga 32 Bora.
0 comments:
Post a Comment