MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Haukuwa ushindi mwepesi, kwani iliwalazimu Yanga kusubiri hadi dakika tatu za mwisho pale mshambuliaji wake tegemeo, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo alipounganisha kwa kichwa krosi ya kiungo Muivory Coast dakika ya 87 kufunga bao hilo pekee.
Kwa ushindi huo, timu ya Wananchi inafikisha pointi 16 katika mchezo wa sita na kusogea nafasi ya pili, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake tisa za mechi nane sasa nafasi ya 11.



.png)
0 comments:
Post a Comment