TIMU za Angola na Zimbabwe zimetoka sare ya kufungana bao 1-1 jioni hii katika mchezo wa Kundi B Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
Mshambuliaji wa Al-Wakrah ya Qatar, Jacinto Muondo ‘Gelson’ Dala alianza kuifungia Palancas Negras dakika ya 24, kabla ya mshambuliaji wa Scottland FC ya kwao, kuisawazishia The Warriors dakika ya 45’+6.
Kwa matokeo hayo, kila timu inaokota pointi ya kwanza baada ya wote kupoteza mechi zao za kwanza, Angola ikifungwa 2-1 na Afrika Kusini na Zimbabwe ikichapwa 3-1 na Misri.
Kwa matokeo hayo, kila timu inaokota pointi ya kwanza baada ya wote kupoteza mechi zao za kwanza, Angola ikifungwa 2-1 na Afrika Kusini na Zimbabwe ikichapwa 3-1 na Misri.

.png)
0 comments:
Post a Comment