• HABARI MPYA

    Tuesday, December 30, 2025

    FEI TOTO AIPELEKA TAIFA STARS 16 BORA AFCON


    TANZANIA imeweka rekodi ya kufuzu Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa mara ya kwanza kihistoria licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na Tunisia katika mchezo wa mwisho wa Kundi C usiku huu Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco.
    Tunisia walitangulia kwa bao la dakika ya 43 la mkwaju wa penalti la kiungo Ismaël Seifallah Gharbi wa Braga ya Ureno anayecheza kwa mkopo FC Augsburg ya Ujerumani. 
    Lakini kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ akaisawazishia Taifa Stars dakika ya 48 na kuivusha Tanzania Hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza ndani ya Fainali nne, zikiwemo za 1980, 2019 na 2023.
    Kwa matokeo hayo, Tunisia imemaliza nafasi ya pili na pointi zake nne, nyuma ya vinara, Nigeria wenye pointi tisa hivyo timu zimefuzu moja kwa moja na Tanzania iliyomaliza na pointi mbili inafuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bora.
    Uganda iliyoshika mkia Kundi C na pointi yake moja safari yake inaishia hapa na wanarejea Kampala kujipanga kwa majukumu mengine.  
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FEI TOTO AIPELEKA TAIFA STARS 16 BORA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top