• HABARI MPYA

    Saturday, December 27, 2025

    TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA UGANDA AFCON


    TANZANIA na Uganda zimegawana pointi kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Kundi C Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) usiku huu Uwanja wa Al Medina Jijini Rabat nchini Morocco.
    Mshambuliaji wa Al Talaba ya Iraq, Simon Happygod Msuva alianza kuifungia Taifa Stars kwa mkwaju wa penalti dakika ya 59, kabla ya mshambuliaji mwingine, Karl Anthony Uchechukwu Mubiru Ikpeazu wa St Johnstone ya Scotland kuisawazishia The Cranes dakika ya 80.
    Karl Anthony Uchechukwu Mubiru Ikpeazu ni mzaliwa wa Harrow, England baba yake akiwa Mnigeria na mama yake Mganda.
    Mshambuliaji wa Vipers SC ha kwao, Uganda Allan Okello alikosa penalti dakika ya 90 baada ya kupiga juu ya lango na kuzima matumaini ya The. Cranes kushinda mechi.
    Kwa matokeo hayo, kila timu inaokota pointi ya kwanza baada ya kupoteza mechi zao za kwanza, Uganda ikifungwa 3-1 na Tunisia na Tanzania ikichapwa 2-1 na Nigeria.
    Msuva amefikia rekodi ya Thuwein Ali Waziri kuifungia jumla mabao matatu Tanzania kwenye Fainali za AFCON akiwa amefikisha idadi hiyo katika Fainali tatu, 2019 Misri, 2023 Ivory Coast na za mwaka huu Ivory Coast.
    Thuwein yeye alifunga mabao yake yote kwenye Fainali za mwaka 1980 nchini Nigeria. 



    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA UGANDA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top