KLABU ya Yanga imemtambulisha mshambuliaji chipukizi, Emmanuel Samuel Mwanengo (22) kuwa mchezaji wake mpya akijiunga na timu hiyo kutoka TRA United ya Tabora.
Mwanengo aliibukia Nyangobo FC ya Zanzibar kabla ya kwenda Tajikistan mwaka 2023 ambako alichezea Ravshan Kulob na Vakhsh mwaka 2024, kabla ya kurejea nchini mwaka huu kujiunga na TRA United, zamani Tabora United.
Na baada ya kuonyesha uwezo wake katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ndani ya Nusu msimu anahamia kwa Wananchi kuendeleza kampeni ya kushinda mataji.



.png)
0 comments:
Post a Comment