• HABARI MPYA

    Saturday, December 27, 2025

    SENEGAL NA DRC ZATOSHANA NGUVU, SARE 1-1 AFCON


    TIMU za Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimetoa sare ya kufungana bao 1–1 katika mchezo wa Kundi D Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku huu Uwanja wa Tangier Grand mjini Tangier nchini Morocco.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na Refa Lahlou Benbraham wa Algeria, mshambuliaji wa Real Betis ya Hispania, Cédric Bakambu alianza kuifungia DRC dakika ya 61, kabla ya mshambuliaji mwingine, Sadio Mane wa Al-Nassr ya Saudi Arabia kuisawazishia Senegal dakika ya 69.
    Kila timu inafikisha pointi nne bada ya kushinda mechi zao za kwanza za Kundi hilo, Senegal ikiichapa Botswana 3-0 na DRC ikiichapa Benin 1-0.
    Baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Botswana leo, Benin inakaa nafasi ya tatu nyuma ya Senegal na DRC katika Kundi D kuelekea mechi za mwisho. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SENEGAL NA DRC ZATOSHANA NGUVU, SARE 1-1 AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top