MSIMU uliopita ikiwa inajulikana kama Tabora United – sasa TRA United iliifunga Yanga mabao 3-1 chini ya kocha Miguel Angel Gamondi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na baada ya mchezo huo akafukuzwa kazi.
Leo, TRA United imerudia tena ubabe wake kwa timu anazoziongoza Gamondi baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 3-1 Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya TRA United leo yamefungwa na kiungo mshambuliaji Mzambia, Chanda Chewe dakika ya 11, mshambuliajin Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 82 na beki Muivory Coast, Anthony Urbain Tra Bi Tra aliyejifunga dakika ya 87, wakati bao la kufutia machozi la Singida Black Stars limefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama dakika ya 54.
Kwa ushindi huo, TRA United inayofundishwa na Kocha Mrundi, Ettienne Ndayiragijje inafikisha pointi tisa katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya tisa, wakati Singida Black Stars inabaki na pointi zake nane za mechi tano sasa nafasi ya 10.



.png)
0 comments:
Post a Comment