TIMU ya Atalanta jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea FC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa New Balance Arena Jijini Bergamo, Italia.
Mabao ya Atalanta yamefungwa na mshambuliaji Gianluca Scamacca dakika ya 55 na kiungo mshambuliaji Mbelgiji, Charles De Ketelaere dakika ya 83, wakati bao pekee la Chelsea limefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Joao Pedro dakika ya 25.
Kwa ushindi huo, Atalanta inafikisha pointi 13 na kupanda nafasi ya tatu, wakati Chelsea inabaki na pointi zakde 10 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi sita.



.png)
0 comments:
Post a Comment