• HABARI MPYA

    Wednesday, December 24, 2025

    MO ACHOURI APIGA MBILI TUNISIA YAICHAPA UGANDA 3-1 AFCON


    TUNISIA imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Olimpiki Jijini Rabat nchini Morocco.
    Mabao ya Eagles of Carthage yamefungwa na viungo, Ellyes Joris Skhiri wa Eintracht Frankfurt ya Ujerumani dakika ya 10 na Mohamed Elias Achouri wa FC Copenhagen ya Denmark mawili dakika ya 40 na 64, wakati la The Cranes lilifungwa na mshambuliaji wa APR ya Rwanda, Denis Omedi dakika ya  90’+2. 
    Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi C jana Nigeria iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco. 
    Mabao ya Super Eagles yalifungwa na beki wa Hull City ya England, Oluwasemilogo Adesewo Ibidapo "Semi" Ajayi dakika ya 36 na winga wa Atalanta ya Italia, Ademola Lookman Olajade Alade Ayoola Lookman dakika ya 52, wakati la Taifa Stars limefungwa na kiungo wa Floriana ya Malta, Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 50.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MO ACHOURI APIGA MBILI TUNISIA YAICHAPA UGANDA 3-1 AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top