• HABARI MPYA

    Sunday, December 28, 2025

    SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA MLANDEGE 3-1 MAPINDUZI CUP


    MABINGWA watetezi, Mlandege SC wameanza vibaya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Singida Black Stars leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
    Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na viungo Muivory Coast, Idriss Diomande, Mghana Emmanuel Kwame Keyekeh na mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Guede Gnadou wakati bao pekee la Mlandege SC limefungwa na Said Matola.
    Timu nyingine kwenye Kundi hilo ni Azam FC na URA FC ya Uganda, wakati Kundi B linazikutanisha timu za Fufuni ya Pemba,  Simba SC ya Dar es Salaam na Mwembe Makumbi City wa Unguja.
    Katika michuano hiyo itakayofikia tamati Januari 13, 2026, Kundi C wapo mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, KVZ ya Unguja na TRA United ya Tabora.
    Mshindi wa kwanza na wa pili wa Kundi A watafuzu Nusu Fainali, wakati Kundi B na C ni vinara tu watasonga mbele kuwania tiketi ya Fainali.
    Mechi zote hadi za Nusu Fainali zitakazochezwa Januari 8 na 9 zitafanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja kasoro Fainali pekee itapigwa Uwanja wa Gombani, Pemba Januari 13, 2026.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA MLANDEGE 3-1 MAPINDUZI CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top