TIMU za Ivory Coast na Cameroon zimegawana pointi baada ya sare ya kufungana bao 1–1 katika mchezo wa Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Marrakech mjini Marrakech nchini Morocco.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Refa Mustapha Ghorbal wa Algeria, winga wa Manchester United, Amad Diallo alianza kuifungia na Ivory Coast dakika ya 51, kabla ya beki mwingine, Ghislain N'Clomande Konan wa Gil Vicente ya Ureno kujifunga dakika ya 56 kuipatia Cameroon bao la kusawazisha.
Kwa matokeo hayo, timu zote inafikisha pointi nne zikiendelea kuongoza zikifuatiwa na Msumbiji yenye pointi tatu, wakati Gabon haina pointi hata moja baada ya mechi mbili za kwanza.



.png)
0 comments:
Post a Comment