WENYEJI, Real Madrid jana wamechapwa mabao 2-1 na Manchester City ya England katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
Real Madrid waliuanza vizuri mchezo na kupata bao la kuongoza dakika ya 28 lililofungwa na winga Mbrazil, Rodrygo Silva de Goes, kabla ya beki Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Nico O'Reilly kuisawazishia Manchester City dakika ya 35 na mshambuliaji Mnorway, Erling Braut Haaland kufunga la ushindi dakika ya 43.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya nne, wakati Real Madrid inabaki na pointi zake 12 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi sita.



.png)
0 comments:
Post a Comment