TIMU ya Wavulana ya Tanzania imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Mashindano ya Ubingwa wa Shule za Afrika kanda ya CECAFA baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini jiini ya leo Uwanja wa St. Mary's-Kitende, Wakiso, Barabara ya Entebbe, Uganda.
Kwa ushindi huo, vijana wa Tanzania chini ya Kocha Boniphace Pawasa wanamaliza hatua ya awali na pointi nne kufuatia jana kuchapwa 1-0 na Ethiopia na kutoa sare ya 0-0 na Rwanda hapo hapo Uwanja wa St. Mary's-Kitende.
Timu ya wasichana ya Tanzania jana ilijihakikishia tiketi ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo ya African Schools Football Championship CECAFA Zone (ASFCCQ) baada ya kuichapa Sudan Kusini 2-1 na Djibouti 6-0 Uwanja wa FUFA Kadiba, Mengo, Rubaga Jijini Kampala nchini Kampala, Uganda.



.png)
0 comments:
Post a Comment