TIMU ya Burkina Faso imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya Equatorial Guinea jioni ya leo Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Mabao ya The Stallions yamefungwa na winga wa Seattle Sounders FC ya Marekani, Georgi Minoungou dakika ya 90’+5 na beki wa kati wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Edmond Fayçal Tapsoba dakika ya 90’+8, wakati la limefungwa na beki wa kati pia wa SS Reyes ya Hispania, Marvin José Anieboh Pallaruelo dakika ya 85.



.png)
0 comments:
Post a Comment