BINGWA wa zamani wa ndondi za kulipwa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua (36) amepata ajali ya gari kwenye barabara kuu ya jimbo la Ogun-Lagos nchini Nigeria.
Muingereza huyo mwenye asili ya Nigeria ndugu zake wanaishi Sagamu, mji ulioko katika Jimbo la Ogun, Kusini-Magharibi mwa Nigeria.
Polisi wanathibitisha kwamba Joshua alikuwa na majeraha madogo lakini "yuko sawa".
Picha na video mtandaoni zinaonyesha kile kinachoonekana kuwa gari lililoharibika.
Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zinasema watu wawili walifariki katika ajali hiyo.
Shahidi Adeniyi Orojo aliambia gazeti la Nigeria The Punch kwamba Lexus na Pajero zilihusika katika ajali hiyo.
"Joshua alikuwa amekaa nyuma ya dereva, na mtu mwingine kando yake," aliambia gazeti hilo.
"Pia kulikuwa na abiria ameketi kando ya dereva, na kufanya watu wanne ndani ya Lexus iliyoanguka. Walinzi wake walikuwa kwenye gari nyuma yao kabla ya ajali hiyo."
Tumepokea taarifa kutoka kwa Kamandi ya Polisi ya Jimbo la Ogun, ambayo inathibitisha watu wawili walifariki katika ajali hiyo ambayo pia ilimjeruhi Anthony Joshua.
Joshua na watu wengine waliojeruhiwa wamepelekwa "hospitali isiyojulikana".
Saa chache kabla ya ajali hiyo, yapata saa Saa 3:30 asubuhi Joshua alichapisha video kwenye Instagram yake akicheza tenisi ya mezani na mwanaume mwingine.
Joshua amekwenda nchini Nigeria kufuatia pambano lake la hivi karibuni dhidi ya Jake Paul Desemba 19 - lakini haijulikani haswa ni wapi au lini video ya tenisi ya mezani ilipigwa.






.png)
0 comments:
Post a Comment