• HABARI MPYA

    Saturday, December 06, 2025

    PAMBA NA PRISONS HAKUNA MBABE, ZATOKA SULUHU SOKOINE


    WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya bila mabao na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Kwa matokeo hayo, Pamba Jiji FC wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa nane, ingawa wanabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa LIgi Kuu nyuma ya JKT Tanzania yenye pointi moja zaidi na mchezo mmoja zaidi wa kucheza kadhalika.
    Kwa upande wao Tanzania Prisons wanafikisha pointi saba katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya 12 mbele ya Azam FC yenye pointi sita za mechi nne hadi sasa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAMBA NA PRISONS HAKUNA MBABE, ZATOKA SULUHU SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top