KLABU ya Yanga Princess imemsajili kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Asha Djafari Djuma (27) kutoka mahasimu, Simba Queens.
Yanga imechapisha picha ya mchezaji huyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiambatanisha na ujumbe; “Asha Djafar ni Mwananchi,” yaani amejiunga nao.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya wanawake ya Burundi, Asha alijiunga na Simba Queens msimu wa 2020/2021 na tangu hapo amekuwa tegemeo la safu ya ushambuliaji ya Malkia wa Msimbazi.



.png)
0 comments:
Post a Comment