• HABARI MPYA

    Tuesday, December 02, 2025

    ONANA ATEMWA KIKOSI CHA CAMEROON AFCON


    KIPA Andre Onana ameachwa nje ya kikosi cha Cameroon kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) - huku timu ikiwa katika machafuko baada ya kocha mkuu Marc Brys kufukuzwa kazi kutokana na madai ya "ujanja".
    Siku chache baada ya kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto'o na Kamati yake ya Utendaji walitangaza kufukuzwa kazi kwa Brys katika taarifa ya kusisimua., nje
    Ikiwa na orodha ndefu ya tuhuma za "kufeli kitaaluma" zilizoelekezwa kwa Brys, ikiwa ni pamoja na "kuwachochea" wachezaji kuipinga FECAFOOT.
    Mbelgiji huyo - aliyeteuliwa na Wizara ya michezo ya Cameroon mnamo Aprili 2024, uamuzi ambao Eto'o alijaribu kuubadilisha mara moja - pia anatuhumiwa kwa "kushirikiana kikamilifu na watu wasiojulikana ndani ya FECAFOOT".
    Pia anatuhumiwa kwa kushindwa kuhudhuria mikutano, kukataa kuweka wazi programu zake za mazoezi, kuhatarisha uhusiano na wadhamini, kutotaja kikosi chake kwa wakati na kutumia "ujanja kukwepa wajibu wake wa kitaaluma wa kufanya mikutano na waandishi wa habari".
    Nafasi ya Brys imechukuliwa na mmoja wa wasaidizi wake, David Pagou, kocha mzoefu wa Cameroon ambaye amewahi kufundisha timu kadhaa katika daraja la juu nchini humo.
    Lakini kikosi cha wachezaji 28 cha Pagou kwa ajili ya AFCON ijayo nchini Morocco, itakayoanza Desemba 21 kinakosa majina kadhaa maarufu — Mbali na Onana wengine ni Nahodha wa timu Vincent Aboubakar, kiungo wa Napoli Andre-Frank Zambo Anguissa na beki Michael Ngadeu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ONANA ATEMWA KIKOSI CHA CAMEROON AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top