KIPA wa Yanga SC, Djigui Diarra ameisaidia Mali kufuzu Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya sare ya bila mabao na Comoro katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Mechi nyingine ya Kundi A jana wenyeji, Morocco walishinda 3-0 dhidi ya Zambia - mabao ya mshambuliaji wa Olympiacos ya Ugiriki, Ayoub El Kaabi mawili dakika ya tano na 50 na winga wa Real Madrid ya Hispania, Brahim Abdelkader Díaz dakika ya 27.
Kwa matokeo hayo, Mali inamaliza na pointi tatu katika nafasi ya pili nyuma ya Morocco iliyofuzu na pointi zake saba, wakati Comoro na Zambia kila moja imemaliza na pointi mbili.
Morocco na Mali zinafuzu moja kwa moja hatua ya 16 Bora, huku Comoro na Zambia zikiaga mashindano.



.png)
0 comments:
Post a Comment