• HABARI MPYA

    Wednesday, December 31, 2025

    SENEGAL, DRC NA BENIN NAZO ZOTE ZAFUZU 16 BORA AFCON


    TIMU za Senegal, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Benin zimefuzu Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya mechi za mwisho za Kundi D usiku wa jana nchini Morocco.
    Senegal iliichapa Benin 3-0, mabao ya beki wa Maccabi Haifa ya Israel, Abdoulaye Seck dakika ya 38 na washambuliaji Mouhamadou Habibou "Habib" Diallo wa Metz ya Ufaransa dakika ya 62 na Pape Cherif Ndiaye wa Samsunspor ya Uturuki dakika ya 90'+7 kwa penalti Uwanja wa Tangier Grand mjini Tangier.
    Nayo DRC iliichapa Botswana 3-0 pia, mabao ya mshambuliaji, Nathanaël Mbuku Wa Mbuku wa FC Augsburg ya Ujerumani anayecheza kwa mkopo Montpellier ya Ufaransa dakika ya 31 na winga wa  Sakaryaspor ya Uturuki, Gael Romeo Kakuta Mambenga mawili dakika ya 41 kwa penalti na 60 Uwanja wa Al Medina Jijini Rabat.


    Kwa matokeo hayo, Senegal imeongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikiizdi tu wastani wa mabao DRC na zote zimefuzu zikiungana na Benin ambayo kwa kumaliza nafasi ya tatu na pointi zake tatu imefuzu kama moja ya timu zilizomaliza nafasi ya tatu na wastani mzuri wa matokeo, nyingine ni Msumbji, Sudan na Tanzania.  
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SENEGAL, DRC NA BENIN NAZO ZOTE ZAFUZU 16 BORA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top