WENYEJI, Azam FC wametoa sare ya bila mabao na Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo baina yao timu hizo mbili za Tanzania zinazoshiriki hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika — Azam FC inafikisha pointi sita katika mchezo wa nne na Singida Black Stars pointi nane katika mchezo wa nne pia.
Wakati Azam FC imeshinda mechi moja na kutoa sare tatu hadi sasa chini ya kocha Mkongo Jean-Florent Ibenge — Muargentina Miguel Angel Gamondi ameiwezesha Singida Black Stars kushinda mechi mbili na kutoa sare mbili hadi sasa.



.png)
0 comments:
Post a Comment