TIMU ya Uganda jana ilitupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Nigeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi C Uwanja wa Fez mjini Fez nchini Morocco.
Mabao ya Super Eagles yalifungwa na mshambuliaji wa Trabzonspor ya Uturuki, Ebere Paul Onuachu dakika ya 28 na kiungo wa Club Brugge ya Ubelgiji, Raphael Onyedika Nwadike mawili dakika ya 62 na 67, wakati bao pekee la The Cranes limefungwa na mshambuliaji wa Vardar ya Macedonia, Rogers Mato Kassim dakika ya 75.
Kwa matokeo hayo, Nigeria inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Tunisia yenye pointi nne na zote zinafuzu moja kwa moja Hatua ya 16 Bora.
Tanzania iliyomaliza nafasi ya tatu na pointi zake mbili inafuzu kama mmoja wa washindi wa tatu bora, huku Uganda iliyoshika mkia Kundi C na pointi yake moja safari yake inaishia hapa.



.png)
0 comments:
Post a Comment