TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Morice Abraham dakika ya 27, mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 38 na winga Mkenya, Mohamed Bajaber dakika ya 85.
Mbeya City ilicheza pungufu kuanzia dakika ya 28 kufuatia mshambuliaji wake tegemeo, Vitalis Mayanga kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa nne na kusogea nafasi ya nne, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake nane za mechi 10 sasa nafasi ya 11 kwenye Ligi ya timu 16.



.png)
0 comments:
Post a Comment