TIMU ya Sudan imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea katika mchezo wa Kundi E Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 usiku huu Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Messie Nkounkou wa Kongo-Brazzaville, bao pekee la Sudan limefungwa na beki wa Torino FC ya Italia, Saúl Basilio Coco-Bassey Oubiña mzaliwa wa Hispania aliyejifunga dakika ya 74'.
Kwa ushindi huo, Sudan inabeba pointi tatu za kwanza katika mchezo wa pili kufuatia kufungwa 3-0 na Algeria kwenye mchezo wa kwanza.
Kwa upande wao Equatorial Guinea wanafikisha mechi mbili za kucheza bila pointi hata moja kufuatia kufungwa 2-1 na Burkina Faso kwenye mchezo wa kwanza.



.png)
0 comments:
Post a Comment