TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji mpya, Jephte kitambala Bola aliyesajiliwa kutoka AS Maniema Union ya kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 81 na winga Iddi Suleiman Nado dakika ya 89.
Wawili hao wote walifunga mabao yao wakimalizia kazi nzuri za kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun Hamoud aliyetokea benchi dakika ya 67 kuchukua nafasi ya winga Zidane Sereri.
Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi tisa na kusogea nafasi ya tisa, wakizidiwa pointi tatu tu na Simba SC baada ya timu zote kucheza mechi tano hadi sasa.



.png)
0 comments:
Post a Comment