• HABARI MPYA

    Saturday, December 06, 2025

    WASICHANA WANG’ARA, WAVULANA MAMBO MAGUMU MICHUANO YA SHULE CECAFA


    TIMU ya wasichana ya Tanzania imeshinda mechi zake zote mbili za Mashindano ya Ubingwa wa Shule za Afrika kanda ya CECAFA, wakati wavulana wamefungwa moja na kutoa sare moja.
    Michuano hiyo ya African Schools Football Championship CECAFA Zone (ASFCCQ ) upande wa wasichana Tanzania ilianza kwa kuichapa Sudan Kusini 2-1, kabla ya kuitandika Djibouti 6-0 Uwanja wa FUFA Kadiba, Mengo, Rubaga Jijini Kampala nchini Kampala, Uganda.
    Wavulana walianza kwa kuchapwa 1-0 na Ethiopia kabla ya kutoa sare ya 0-0 n Rwanda Uwanja wa St. Mary's-Kitende, Wakiso, Barabara ya Entebbe, Uganda. 


    Michuano hiyo itaendelea kesho na wavulana watakamilisha mechi zao za Hatua ya awali kwa kumenyana na Sudan Kusini hapo hapo  St. Mary's-Kitende na wasichana watamenyana na Ethiopia hapo hapo Uwanja wa FUFA Kadiba.
    Nusu Fainali zitafuatia Jumatatu na Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu ni Jumanne.
    Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha CECAFA katika mashindano ya Afrika. 
    Ikumbukwe Tanzania ndio mabingwa wa Afrika kwa wanaume na kwa wasichana bingwa ni Ghana. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASICHANA WANG’ARA, WAVULANA MAMBO MAGUMU MICHUANO YA SHULE CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top