• HABARI MPYA

    Tuesday, December 02, 2025

    TANZANIA BINGWA MICHUANO YA CECAFA U17


    TANZANIA imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya CECAFA baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Uganda jioni ya leo Uwanja Abebe Bikila nchini Ethiopia.
    Mabao ya Serengeti Boys kwenye mchezo huo wa michuano ya kufuzu Fainali za Afrika ‘U17 AFCON CECAFA Qualifiers’ yamefungwa na Razak Juma Mbegelendi dakika ya sita na 30 na Luqman Mbalasalu dakika ya 45, wakati ya Uganda yamefungwa na Thomas Ogema dakika ya 13 na Brian Olwa dakika ya 90’+6.
    Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, wenyeji Ethiopia waliichapa Kenya 3-0, mabao ya Dawit Kassaw dakika ya 67, Binyam Abrha dakika ya 79 na Biruk Eyirachew dakika ya 90’+3.
    Pamoja na kufungwa, Uganda mabingwa wa msimu uliopita wanaungana na Tanzania na washindi wa tatu, Ethiopia kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 mwakani nchini Morocco.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA BINGWA MICHUANO YA CECAFA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top