• HABARI MPYA

    Tuesday, January 20, 2026

    JKT TANZANIA YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 1-0


    TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 81 na kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 11 na kurejea kileleni, ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi nne mkononi.
    Kwa upande wao Singida Black Stars wanabaki na pointi zao tisa za mechi saba nafasi ya 11 kwenye Ligi ya timu 16.
    Baada ya mchezo huo, Singida Black Stars wanakwenda Zanzibar kuwasubiri AS Otoho ya Kongo-Brazzaville katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Jumapili Uwanja wa New Amaan Complex.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKT TANZANIA YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top