TIMU ya Wasichana ya Tanzania imefanikiwa kwenda Fainali ya Mashindano ya Ubingwa wa Shule za Afrika kanda ya CECAFA baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burundi leo Uwanja wa FUFA Kadiba, Mengo, Rubaga Jijini Kampala nchini Kampala, Uganda.
Tanzania sasa itakutana na Ethiopia katika Fainali kesho ambayo leo imeitoa Uganda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya bila kufungana kwenye mchezo mwingine wa Nusu Fainali za Wasichana.
Habari mbaya kwa Wavulana wa Tanzania wamefungwa 2-0 na Uganda katika Nusu Fainali Uwanja wa St. Mary's-Kitende, Wakiso, Barabara ya Entebbe, Uganda.
Tanzania itawania nafasi ya tatu dhidi ya Burundi ambayo imefungwa kwa penalti 13-13 na Ethiopia katika Nusu Fainali nyingine ya Wavulana leo.
Fainali ya Wavulana ni Uganda Ethiopia na Bingwa kwa Wavulana na Wasichana watafuzu Fainali za Afrika na Mashindnao ya Shule ambazo zitafanyika mwakani.



.png)
0 comments:
Post a Comment