MSHAMBULIAJI Mbrazil, Raphinha jana alifunga mabao yote mawili FC Barcelona ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Osasuna katika mchezo wa La Liga Uwanja wa Spotify Camp Nou.
Kwa ushindi huo, Bacelona inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza La Liga kwa pointi saba zaidi ya Real Madrid ambao wana mechi moja mkononi na leo wanacheza na Alavés Uwanja wa Mendizorroza.



.png)
0 comments:
Post a Comment