TIMU ya Azam FC imepangwa Kundi A katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar pamoja na mabingwa watetezi, Mlandege SC, Singida Black Stars na URA ya Uganda.
Katika michuano hiyo itakayoanza Desemba 28, Simba SC wamepangwa Kundi B Pamoja na Mwembe Makumbi City ya Unguja na Fufuni FC ya Pemba, wakati watani wao, Yanga wapo Kundi C pamoja na KVZ ya Unguja na TRA United ya Tabora.
Mshindi wa kwanza na wa pili wa Kundi A watafuzu Nusu Fainali, wakati Kundi B na C ni vinara tu watasonga mbele kuwania tiketi ya Fainali.
Mechi zote hadi za Nusu Fainali zitakazochezwa Januari 8 na 9 zitafanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja kasoro Fainali pekee itapigwa Uwanja wa Gombani, Pemba Januari 13, 2026.



.png)
0 comments:
Post a Comment